Chuo kikuu cha Alkafeel kimeingia katika usanifu wa (Times Higher Education Impact Rankings)

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel kimeingia kwenye usanifu wa (Times Higher Education Impact Rankings) katika mwaka wa masomo 2020m, kimepata nafasi ya sita kwa ubora katika vyuo vikuu vya Iraq, miongoni mwa vyuo kumi na nane na nafasi ya (601) kimataifa.

Huzingatiwa mambo mengi katika swala hili, ikiwa ni pamoja na uwezo, uwadilifu na uimara wa taasisi, huu ni usanifu wa mara ya nne ambao chuo hiki kinashiriki, hapo awali kilishiriki katika usanifu wa (Webometrics) na usanifu wa (RUR) na (GreenMetrics).

Kuhusu kuingia kwa chuo kikuu cha Alkafeel katika usanifu huu tumeongea na raisi wa chuo Dokta Nuris Muhammad Shahidi Dahaan amesema kua: “Hakika chuo kikuu cha Alkafeel kinafuata utaratibu kilio jiwekea ili kukifanya kuwa chuo bora chenye kutoa elimu nzuri katika taifa letu kipenzi.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya kila aina ya juhudi kuboresha sekta zake, kielimu, kitamaduni, kimalezi na kufanya tafiti za kielimu hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: