Kwa video: shirika la Khairul-Juud limetengeneza soksi za mikononi zenye ubora mkubwa

Maoni katika picha
Shirika la Khairul-Juud limetengeneza bidhaa bora ya kuvaa mikononi kwa ajili ya kujikinga na bakteria, bidhaa hiyo inatokana na utafiti uliofanywa na kituo hicho katika maabara zake.

Mkuu wa shirika la Khairul-Juud Mhandisi Maitham Bahadeli ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Shirika la Khairul-Juud lina maabara tatu, kuna maabara ya kemia, bailojia na maabara ya tafiti na maboresho, ambazo hufanya kazi ya kuboresha bidhaa zake wakati wote”.

Akaongeza kua: “Maradhi haya husababishwa na virusi, kwa hiyo tumetengeneza kifaa chenye uwezo mkubwa wa kuzuwia virusi na bakteria halafu kinauzwa kwa bei nafuu”.

Tambua kua shirika la Khairul-Juud lilitangaza kuongeza utengenezaji wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona mara tano zaidi, kwa ajili ya kugawa kwa wananchi na vituo vya afya hapa Karbala na mikoani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: