Muhimu: Viongozi wa Hashdi Shaábi wamesisitiza kuendelea kusaidia watu wanaojitolea

Maoni katika picha
Viongozi wa Hashdi Shaábi zilizo undwa na Ataba takatifu ambazo ni –Imamu Ali, Abbasi Qitaliyya na Liwaau Ali Akbaru na Answaru Marjaiyya- wenye namba (2, 11, 26, 44), jioni ya Alkhamisi ya mwezi (29 Shabani 1441h) sawa na (23 Aprili 2020m) wamehamia katika Hashdi Shaábi kupitia namba (946/6D/S/W/R/M) tarehe (19/04/2020m) kufuatia taarifa ya kamanda mkuu iliyo tangazwa kwenye vyombo vya habari jana.

Akabainisha kua wanaangalia uwezekano wa vikosi vingine vinavyo penda kujiunga chini ya taratibu za kitaifa, na misingi ya kisheria, wataendelea kuwasiliana na viongozi wa hashdi kwa ajili ya kuratibu mabadiliko.

Wakasisitiza kua wataendelea kusaidia watu wanaojitolea kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu kwa kuwapa mafunzo na huduma za kibinaadamu na kitiba pamoja na mambo mengine.

Akasema kua mabadiliko hayabadilishi ushirikiano wa vikosi, akasisitiza kua wote ni wazalendo na wanafanya kinacho hitajika na taifa lao, hakuna yeyote mwenye mtazamo mbaya dhidi ya mwingine, kinacho fanyika ni kurekebisha baadhi ya mambo, na kulinda taifa tukufu (ardhi, raia na maeneo matakatifu), chini ya wito wa haki, hekima na ubinaadamu uliotolewa na Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani.

Wakasisitiza kua mambo yote yanafanywa chini ya usimamizi wa Mheshimiwa Rais wa nchi Baraham Swalehe, na jemedari mkuu Dokta Aadil Abdulmahdi pamoja na baadhi ya makamanda wa jeshi, sambamba na mawakili wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, tunawaahidi raia wetu wapenzi kua tunaunda chombo kimoja imara cha ulinzi ambacho ni ngome madhubuti ya taifa letu katika utowaji wa huduma na ulinzi.

Tunashukuru vyombo vyote vya dini, serikali na taasisi mbalimbali zinazo unga mkono mradi huu mtukufu, pia tunawatakia rehema mashahidi watukufu wa taifa hili na kuwaombea kupona haraka majeruhi watukufu, tunamuomba Mwenyezi Mungu alipe amani taifa letu pamoja na mataifa mengine na atulinde dhidi ya janga la Korona, hakika yeye ndiye mbora wa kuneemesha na muweza wa kunusuru.

Kuangalia nakala ya tamko tazama picha iliyo ambatanishwa na habari hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: