Kwa video.. Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu amesema: Namnagani tunaupokea mwezi wa Ramadhani katika zama hizi za Korana?

Maoni katika picha
Tupo mwanzoni mwa mwezi wa rehema na maghafira –mwezi mtukufu wa Ramadhani- Wakili wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ameeleza umuhimu wa kujiandaa kinafsi, kiroho na kiakili katika kuupokea mwezi mtukufu, na kunufaika nao kwa sababu huu ni mwezi bora, mwezi wa baraka, ni fursa ambayo yatupasa kuitumia vizuri.

Akaelezea hali ya sasa ya mabambano dhidi ya virusi vya Korona, akafupisha kwa kuongea nukta mbili muhimu:

Kwanza: Watu wanalazima kuzingatia na kufuata maelekezo ya kujikinga na maambukizi yanayo tolewa na wataalamu wa afya, walinde usalama wao na afya zao, wasijiingize kwenye hatari au kuwaingiza wengine kwenye hatari, lazima tufuate maelekezo hayo na hakuna ruhusa kwa yeyote kudhuru afya yake au afya za watu wengine.

Pili: Wahudumu wa afya wamefanya kazi kubwa na bado wanaendelea na kazi, wanatakiwa kuwa na kauli moja ili kutowachanganya watu, lazima kuwe na msemaji maalum, wala wasikubali kauli zinazotolewa na wasiokua wataalamu, taarifa zote zitolewe kwa kufuata misingi ya elimu na wala zisikuzwe na vyombo vya habari vya kisasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: