Mradi wa mafaili ya waandisi wa kiiraq umekusanya katika mtandao wake zaidi ya waandishi (6500) wa vitabu

Maoni katika picha
Mradi wa kukusanya waandishi wa vitabu wa kiiraq katika kituo cha faharasi na upangiliaji wa taarifa chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, umekusanya zaidi ya waandishi (6500) katika mtandao wake maalum, baada ya kumaliza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake, nao ni mtandao wa pekee katika nchi za kiarabu.

Mkuu wa kituo cha faharasi na upangiliaji wa taarifa Ustadh Hasanaini Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Baada ya kupata wazo la kukusanya waandisi wa vitabu wa kiiraq, tulilifanyia kazi na tukafanikiwa kufungua toghuti chini ya mwaka mmoja, ambayo tumekusanya taarifa za waandishi hao na vitabu vyao na historia zao kamili”.

Akaongeza kua: “Toghuti inaelekeza sehemu vinapo patikana vitabu hivyo katika maktaba za hapa Iraq, ili kumrahishishia msomaji”.

Akaendelea kusema: “Baada ya kumaliza mwaka wa kufanya kazi mfululizo tumefanikiwa kukusanya zaidi ya waandishi (6500) wa kiiraq, ambao wameandika zaidi ya vitabu (15000)”.

Akabainisha kua: “Tunaendelea na kazi ya kukusanya majina ya waandishi zaidi wa kiiraq, tumetengeneza faili la kimataifa kama zinavyo fanya nchi nyingi zilizo endelea, jambo hili ni la kwanza na la pekee kufanywa katika nchi za kiarabu”.

Kumbuka kuwa faili la waandishi wa kiiraq linajumuisha vitu vingi, ikiwa ni pamoja na kuzitambulisha maktaba tofauti za Iraq, pia waandishi wanaweza kuweka toghuti zao na majina yao bure kwenye faili hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: