Chuo kikuu cha Ummul-Banina cha wasichana kinatangaza mashindano ya mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) cha wasichana chini ya kitengo cha elimu na utamaduni, kimekusudia kufanya mashindano ya kidini na kitamaduni ndani ya mwezi wa Ramadhani, kupitia toghuti maalum ya chuo pamoja na mitandao ya mawasiliano ya kijamii iliyo chini yake.

Mkuu wa chuo Shekh Hussein Turabi ameaongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu mashindano hayo, amesema kua: “Mashindano haya ni sehemu ya harakati za chuo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akaongeza kuwa: “Kuendesha mashindano kwa njia ya masafa (mtandao) kutafanyika kwa kutumia toghuti maalum ya chuo pamoja na mitandoa ya mawasiliano ya kijamii iliyo chini yake”.

Akafafanua kuwa: “Mashindano yatakuwa kama ifuatavyo:

  • 1- Shindano la mjukuu mkubwa (Sibtu-Akbaru) la kuhifadhi khutuba na kauli za Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa ajili ya kutambua hadithi muhimu zilizo pokewa kutoka kwa Imamu Hassan (a.s) na kuchukua mazingatio na mafunzo kwenye hadithi hizo.
  • 2- Shindano la (Shadhraati Ramadhwaniyyah) litakua na maswali ya aina tatu (Fiqhi, Aqida na mambo mengine).
  • 3- Shindano la (Swafahaatu Mushriqah) la kuandika visa vya kweli kuhusu fatwa ya jihadi kifaya na fatwa ya kutoshelezeana (Atakaaful-Ijtimaai) vinavyo onyesha ujasiri na ushujaa wa wapambanaji na kuwafanya waendelee kuonekana wakati wote, sambamba na kupata mazingatio na mafunzo kwenye visa hivyo kwa vizazi vijavyo.
  • 4- Shindano la (Fiqhu-Swiyaami) linahusu funga na hukumu zake, kila siku yataulizwa maswali kutoka kwenye kitabu cha Minhaaju Swalihina.. Kitabu Swaumu.
  • 5- Shindano la (Fas-alu-Ahladhikri) linahusu kutuma aya na tafsiri yake pamoja na kuuliza swali maalum kwa ajili ya kupata muongozo na nuru ya Quráni kwa kutambua maana ya aya hiyo kwa undani zaidi”.

Shekh Turabi akasema kunazawadi zimeandaliwa na malalo takatifu kwa washindi watatu wa mwanzo kwenye kila aina ya shindano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: