Kitengo cha habari kimeandaa masafa ya bure kwa ajili ya vipindi vya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi huu mtukufu

Maoni katika picha
Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandaa masafa ya bure yenye ubora mkubwa (Clean), itakayo tumika kurusha vipindi vya Ataba tukufu katika mwezi wa Ramadhani, ambapo kutakuwa na vipindi vya ibada, Quráni, na masomo mbalimbali.

Kitengo cha habari kimetoa wito kwa vyombo vyote vya habari vya kitaifa na kimataifa vinavyo penda kurusha vipindi hivyo watumie anuwani zifuatazo:

Satellite: Eutelsat7A at 7.0 East(W3A)

DOWNLINK:12680.200 H

MOD:DVBS2

QPSK

FEC:5/6

Sr :3250

HD/MPEG-4

Tariba ya vipindi vya Ataba katika mwezi wa Ramadhani itakuwa kama ifuatavyo:

  • - Quráni tukufu na adhana ya Dhuhuraini saa 5:45.
  • - Usomaji wa Quráni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu saa 11:00 Alasiri.
  • - Quráni tukufu na adhana ya Magharibaini saa 12:45.
  • - Duaau-Iftitaahi saa 2:00 jioni.
  • - Muhadhara wa kidini kutoka Atabatu Abbasiyya utakao tolewa na Mheshimiwa Shekh Abduswahibu Twaaiy saa 3:00 jioni.
  • - Kipindi cha meza ya vizito viwili (Maaidatu-Thaqalaini) kipindi cha Quráni yenye vipengele vingi saa 5:00 usiku.
  • - Duaau-Abu Hamza Shimali saa 6:00 katikati ya usiku.
  • - Dua za usiku na adhana ya Alfajiri zitaanza saa 9:15 Alfajiri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: