Kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani: Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) imeanza kufanya shindano la Aashiqiin awamu ya tatu.

Maoni katika picha
Kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani –msimu wa Quráni- Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) na chuo kikuu cha Umul-Banina cha wasichana wanaendesha shindano la usomaji wa Quráni awamu ya tatu.

Shindano hilo ni la kusoma Quráni tukufu na kuelekeza thawabu zake kwenye Maqaam ya Imamu wa zama (a.f).

Shindano limeanza mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani na litaendelea mwezi mzima.

Zawadi za washiriki wa shindano ni:

  • 1- Mshindi wa kwanza: atapewa nakala ya Quráni tukufu (chapa ya Atabatu Abbasiyya) na (dinari laki tano).
  • 2- Mshindi wa pili: atapewa bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) na (nidari laki tatu).
  • 3- Mshindi wa tatu: atapewa pete ya fedha kutoka kwenye kiwanda cha Atabatu Abbasiyya tukufu na (dinari laki mbili).

Zingatia yafuatayo:

  • 1- Mshiriki anahiyari ya kusoma moja kwa moja yeye mwenyewe au kusikiliza visomo vya Quráni vinavyo fanywa na Maahadi wakati wa usiku ndani ya mwezi wa Ramadhani kwenye luninga, redio na mitandao ya mawasiliano iliyo chini ya Maahadi.
  • 2- Unapo maliza kusoma tuna neno tayali (tama).
  • 3- Inafaa kusoma kwa niyaba ya walio hai au waliokufa.

Mshindi wa (kwanza, wa pili na wa tatu) watapatikana kwa kupiga kura baina ya washiriki wa shindano.

Kwa maelezo zaidi piga simu kupitia moja ya namba mbili zifuatazo: (07731881800 / 07805776518)

Au wasiliana nasi kwa njia zifuatazo:

1- facebook.com/TurathAlanbiaa

2- t.me/turathmanage

3- Viber / whatsapp (07731881800).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: