Kisomo cha Quráni katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kinaendelea jirani na malalo ya Abulafadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Alasiri ya Jumamosi ya mwezi mosi Ramadhani katika mazingira mazuri kiroho ndani ya haram takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kimefanywa kisomo cha Quráni chini ya usimamizi wa Maahadi ya Quráni tukufu ambayo ipo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya na kushiriki jopo la wasomaji watukufu, kisomo hicho kitafanyika kila siku hadi mwisho wa mwezi wa Ramadhani.

Mkuu wa Maahadi ya Quráni tukufu Shekh Jawadi Nasrawi amesema kuwa: “Katika usomaji huo wa Quráni tumechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, tutasoma kila siku saa kumi na moja Alasiri na kurushwa kwenye vituo vya luninga tofauti, miongoni mwa vituo hivyo ni: (Kituo cha Alfuraat, kituo cha Alquránul-Kariim, kituo cha Almahdi na kituo cha Al-Aqiilah) pamoja na vituo vingine, wanarusha kupitia masafa ya bure iliyo tengenezwa na kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya, kila siku tunasoma juzuu moja kwa muda wa saa moja”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya mwaka mzima, hufanya semina nyingi na vikao mbalimbali vya usomaji wa Quráni kwa kufuata hukumu za usomaji na tajwidi, kikiwemo kisomo hiki ambacho ni utamaduni wa kila mwaka, kutokana na mazingira ya mwaka huu tumetosheka na kufanya hivi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: