Mkuu wa hospitali ya Hindiyya amesema kuwa: Ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha tatu ni tunda zuri lililoiva kwa muda mfupi

Maoni katika picha
Mkuu wa hospitali ya Hindiyya Dokta Waathiqu Jayati Fadhili Alhasanawi amesema kuwa kituo cha tatu kilicho jengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na juhudi za mafundi wake wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi, wamemaliza ujenzi wa kituo hiki kwa muda mfupi sana, siku ishirini na nne (24) tu, na kuwa sehemu bora ya kutoa huduma katika hospitali kuu ya Hindiyya.

Akaongeza kuwa: “Baada ya kuomba msaada kwa mganga mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel, na maombi yetu kuwasilishwa kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Sayyid Muhammad Ashiqar, maombi yetu yalikubaliwa haraka na mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wakapewa jukumu la kuanza ujenzi, kwa hakika wamekamilisha ujenzi ndani ya muda mfupi, tunatoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na kiongozi wake mkuu wa kisheria pamoja na katibu mkuu, bila kuisahau hospitali ya rufaa Alkafeel na kila aliye changia kufanikisha ujenzi huu”.

Tambua kua Atabatu Abbasiyya imefanya ufunguzi rasmi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika hospitali kuu ya Hindiyya (kituo cha Alhayaat cha tatu) siku ya jana Jumaili ya mwezi (2 Ramadhani 1441h) sawa na tarehe (26 Aprili 2020m) mbele ya waziri wa afya wa Iraq, na hospitali ya rufaa Alkafeel imekitoa zawadi kwa hospitali kuu ya Hindiyya.

Fahamu kuwa kituo hiki kimejengwa kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Korona na kupunguza msongamano katika kituo cha Alhayaat kilichopo katika mji wa Imamu Hussein (a.s), ukizingatia kuwa wilaya ya Hindiyya ni miongoni mwa wilaya kubwa katika mkoa wa Karbala, ipo kilometa (20) kutoka katikati ya mji wa Karbala, mradi huu umejengwa kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala chini ya usimamiaji wa idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: