Waziri wa afya amesema kuwa: Hospitali ya Alkafeel ni kielelezo cha mafanikio ya wairaq na tunatamani kusambaza uzowefu wake kwenye hospitali zote hapa nchini…

Maoni katika picha
Waziri wa afya wa Iraq Dokta Jafari Alawi amesema kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel ni mradi bora, akaomba uzowefu wao uigwe na mikoa yote ya Iraq.

Ameyasema hayo alipo tembelea hospitali hiyo wakati akielekea kwenye ufunguzi wa kituo cha Alhayaat cha tatu, ambacho hospitali ya rufaa Alkafeel imekikabidhi kwa hospitali kuu ya Hindiyya katika mji wa Towareji.

Dokta Jafari Alawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika hospitali ya rufaa Alkafeel ni mradi bora, inatoa huduma nzuri za afya, tunatamani uzowefu wake uigwe na hospitali zote za Iraq kwenye mikoa tofauti”.

Akasisitiza kuwa: “Kuwepo kwa hospitali hii ni kielelezo cha mafanikio ya wairaq katika ujenzi wa taasisi za afya, na kutoa huduma bora bila kuhitaji msaada wan je”.

Kumbuka kuwa waziri wa afya alikuwa amesha tembelea hospitali ya rufaa Alkafeel, akifuatana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar na mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel Dokta Jaasim Ibrahim, ambao walitoa maelezo kwa ufupi kuhusu wasifu wa hospitali na huduma zinazo tolewa katika hospitali hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: