Toleo la tano na sita la jarida la (Alkhazaanah)

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi chini ya Daru Makhtutwaat katika kitengo cha elimu na utamaduni, kimechapisha toleo la (tano na sita) la jarida la (Alkhazaanah), nalo ni moja kati ya majarida ya kielimu yanayo chapishwa na Ataba tukufu, ambalo huandika taarifa za turathi za maandishi na hutoka kila nusu ya mwaka.

Mkuu wa kitengo cha uhariri wa jarida hilo (Alkhazaanah) ustadh Muhammad Wakili ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: Kituo chetu kimechapisha toleo la tano na la sita la jarida la (Alkhazaanah), matoleo hayo yanamilango mitano, mlango wa kwanza ni (tafiti za turathi) wa pili ni (nakala zilizo hakikiwa) na wa tatu ni (kukosoa matokeo ya turathi).

Akaongeza kuwa: “Kuhusu mlango wa nne umejikita katika faharasi za nakala kale (makhtutwaat) na kubaini machapisho, na mlango wa tano na wa mwisho umejikita katika habari tofauti, unaitwa (habari za turathi”.

Kumbuka kuwa jarida la (Alkhazaanah) linachapishwa na kituo cha uhuwishaji wa turathi chini ya Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, nalo ni jarida la kielimu ambalo huchapishwa katikati ya mwaka, huandika kuhusu turathi za maandishi, ni jarida maalumu kwa ajili ya kuandika nakala kale zilizo hakikiwa na taarifa kuhusu turathi za maamdishi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: