App ya (Haqibatulmu-uminu) inaendesha shindano la mwezi wa Ramadhani awamu ya pili

Maoni katika picha
App ya (Haqibatulmu-uminu) iliyo tengenezwa na kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendesha shindano la mwezi wa Ramadhani awamu ya pili, ambalo ni kujibu maswali ya Fiqhi na Ibada za kila wiki kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii (facebook na Instagram) ndani ya mwezi huu wa Ramadhani.

Washindi watatangazwa baada ya kumaliza wiki zote za mwezi mtukufu wa Ramadhani, kila wiki kutakuwa na washindi wanne, kila mmoja atapewa zawadi za kutabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Baada ya kumaliza wiki zote nne za mwezi wa Ramadhani tutakuwa na jumla ya washindi (16), kisha watapigiwa kura na kupatikana washindi watano watakaopewa simu za kisasa.

Kumbuka kuwa App ya (Haqibatulmu-uminu) imefanyiwa marekebisho maalum kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani wa mwaka huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: