Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na idara ya mkoa wa Karbala wanakarabati barabara za mji mkongwe

Maoni katika picha
Mkuu wa idara ya mji mkongwe wa Karbala Mhandisi Abiir Salim Naasir na rais wa kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu Sayyid Naafii Ni’mah Abisi Mussawi, wametembelea barabara na chochoro za mji mkongwe unao zunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuangalia ujenzi wa barabara na njia hizo.

Sayyid Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika ziara hiyo imehusisha sehemu zilizo fanyiwa ukarabati na kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kwa ushirikiano wa Atabatu Abbasiyya tukufu na idara ya mkoa wa Karbala, shughuli hiyo ilihusisha kazi nyingi, miongoni mwa kazi hizo ni kuinua kingo za barabara na mitaa ya mji mkongwe, sambamba na kupanua njia za zamani ili kuwezesha kupita gari zaidi ya moja na kupunguza msongamano katika njia hizo, pamoja na kujenga upya sehemu za milango na vizuwizi vya barabara na vya njia ndogo zinazo elekea katika haram takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Kazi zote zilizo fanywa zimezingatia misingi ya kijamii na amani, kwa mfano kuondoa nyaya za umeme zilizokuwa zimezagaa barabarani na mabango ya maduka na hoteli zilizo fungwa”.

Tambua kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu kinaendelea kutowa huduma tofauti kupitia wataalamu wake, na kimesha fanya miradi mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: