Kwa vifaa vya kisasa: Watumishi wa kikosi cha Abbasi wanaendelea na kazi ya kupuliza dawa katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu na mji mkongwe

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kinaendelea na kazi ya kupuliza dawa barabara na nyumba za mji wa Karbala kwa ajili ya kupambana na virusi vya Korona, safari hii wanatumia vifaa vya kisasa zaidi.

Opresheni ya mwishi iliyo fanywa usiku wa Jumanne ilihusisha eneo la katikati ya haram mbili tukufu pamoja na sehemu zinazo zunguka eneo hilo na sehemu yote ya mji mkongwe.

Kiongozi wa kitengo cha ukaguzi Ustadh Farasi Ghaibu Fadhil, amesema kuwa: “Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) wametumia vifaa vya kisasa zaidi katika opresheni hii, wametumia vifaa vya kubeba vyenye uwezo wa kuingia lita (22)”.

Akaongeza kuwa: “Hivyo ni vifaa bora kushinda vilivyo kuwa vinatumiwa siku za nyuma, vinatowa dawa kwa wingi na inasambaa vizuri kwa kiasi cha mita tatu hadi nne”.

Akasisitiza kuwa: “Tunaendelea na kazi ya kupuliza dawa katika maeneo mengine ya mkoa kama ilivyo pangwa, vifaa hivi vitasaidia sana utendaji wetu”.

Kumbuka kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) kinaendelea kuwahudumia wananchi kwa kushiriki katika opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) au katika opresheni za kupuliza dawa katika maeneo mbalimbali kwenye mikoa tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: