Idara ya shule za Alkafeel za wasichana imeanzisha App ya Haqibatu-Swaaimu

Maoni katika picha
Idara ya shule za Alkafeel za wasichana chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeanzisha App ya (Haqiibatu-Swaaimu) inayo fanya kazi katika simu ganja (smartphone), inahusu ibada za mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kiongozi wa idara tajwa bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kuanzishwa kwa App hii ni sehemu ya harakati za idara katika mwezi wa Ramadhani, na kuongeza uwelewa wa Dini kwa mwanamke wa kiislamu sambamba na kuzipa haki ibada za mwezi huu mtukufu”.

App hiyo inasehemu zifuatazo:

  • 1- Zawadi yako katika mwezi wa Ramadhani.
  • 2- Fatwa za mwezi wa Ramadhani.
  • 3- Tunahuika kwa Quráni.
  • 4- Chakula chako ni roho yangu na mwili wangu.
  • 5- Wanawake wenu ni mbeleko (mahdawiyya).
  • 6- Kujizuwia Ramadhani”.

Akafafanua kuwa: “Kuna milango ya Fiqhi, Ibada na Fikra, yote hayo ni kwa ajili ya kumfanya mwanamke wa kiislamu apate uwelewa mkubwa wa Fiqhi, na ibada katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani”.

Kumbuka kuwa idara ya shule za wasichana Alkafeel imeandaa ratiba rasmi ya mwezi wa Ramadhani kuanzia siku ya kwanza ya mwezi huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: