Chuo kikuu cha Alkafeel kimetangaza punguzo jipya kwa wanafunzi wake

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel ambacho kipo chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza punguzo la ada kwa asilimia kumi (%10) kwenye michepuo na ngazi zote za masomo katika mwaka (2019 / 2020m).

Punguzo hilo ni sehemu ya kuonyesha kushikamana na wanafunzi wake katika mazingira haya magumu ambayo wananchi wanapitia kwa sasa, punguzo lipo kama ifuatavyo:

  • 1- Ada ya masomo katika ngazi zote imepunguzwa mara ya pili kwa asilimia kumi (%10), katika mwaka wa masomo (2019/2020m).
  • 2- Hivyo jumla ya punguzo katika mwaka wa masomo (2019/2020m) linakuwa asilimia ishirini (%20).
  • 3- Mwanafunzi atanufaika na punguzo hilo (lililo tajwa kwenye namba moja) kwa kulipa ada kamili ya masomo kuanzia tarehe (29/04/2020m) hadi mwisho wa mda rasmi wa kazi katika siku ya Jumatano ya tarehe (20/05/2020m).
  • 4- Punguzo la pili (lililo tajwa kwenye namba mbili) halihusishi wanafunzi waliopewa punguzo hapo awali kwa sababu maamum.
  • 5- Wanafunzi watakao chelewa kulipa ada zao baada ya tarehe (20/05/2020m) hawatanufaika na punguzo lililotajwa kwenye namba moja.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed kimetangaza punguzo kama hili, linalo lenga kuwasaidia wazazi wa wanafunzi, kutokana na mazingira magumu mambayo wananchi wanapitia kwa sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: