kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Alkafeel kimeratibu mhadhara wa kimtandao kuhusu faida za kutumia intanet katika kuongeza uwezo wa lugha ya kiengereza

Maoni katika picha
Kitivo cha udaktari wa meno chini ya elimu ya msingi katika idara ya elimu endelevu kwenye chuo kikuu cha Alkafeel, kimeratibu mhadhara kwa njia ya mtandao kuhusu jinsi ya kunufaika na intanet katika kuongeza uwezo ya lugha ya Kiengereza chini ya anuani isemayo (In English Language Learning).

Mhadhara huo unatolewa na mkufunzi muandamizi Qassim Zubaidi na kurushwa mubashara kupitia moja ya mitandao ya mawasiliano ya kijamii kutokana na mazingira ambayo jamii inapitia kwa sasa, mhadhara huo umeshuhudiwa na idadi kubwa ya wakufunzi wa vyuo vingi hapa Iraq.

Amebainishwa kuwa: “Mhadhara ilikuwa unahusu njia muhimu na mtazamo wa kujifunza lugha za kigeni kwa ujumla na kwa namna ya pekee lugha ya kiengereza, pamoja na namna ya kunufaika na intanet katika kuongeza uwezo wa lugha, ukizingatia kuwa intanet inamifumo maalum ya kujinza lugha, tena asilimia kubwa ya mifumo hiyo ni bure, kila mtu anaweza kuitumia bila gharama, akaongea pia kuhusu namna ya kunufaika na mitandao ya mawasiliano ya kijamii katika kuongeza uwezo wa lugha”.

Makamo rais wa kitengo cha taaluma Dokta Nawaal Aaidi Almayali amesema kuwa chuo kinafanya juhudi ya kuendesha nadwa na warsha tofauti, na zingine zitafanyika hivi karibuni Insha-Allah.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kila mwaka hufanya warsha, nadwa, semina pamoja na makongamano ya tafiti chini ya ratiba maalum, kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, chuo kimeamua kuendesha baadhi ya shughuli zake kwa njia ya mtandao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: