Chuo kikuu cha Al-Ameed kimeandaa: Jukwaa la wanafunzi wa vyuo vikuu vya kiarabu na kiajemi

Maoni katika picha
Kutokana na sera ya chuo kikuu cha Al-Ameed ya kujenga uhusiano mwema na vyuo vingine vya kimataifa, na kuimarisha mawasiliano baina ya wanafunzi wa vyuo hivyo, kimeandaa jukwaa la wanafunzi wa vyuo vikuu vya kiarabu na kiajemi kutoka katika nchi za (Qatar, Ukren, China, Hispaniya, Esdonia) jukwaa hilo linaitwa (ZOOM).

Wanafunzi wamepata fursa ya kujadiliana na kubadilishana mawazo katika mambo mbalimbali ya kimataifa, likiwemo janga la virusi vya Korona na athari zake katika kila nchi, sambamba na kujadili dalili za ugonjwa huo na njia za kujikinga zinazo tumiwa na kila taifa, aidha watajadili selebasi za masomo katika kila taifa na utaratibu wa masomo ya mtandaoni.

Mkutano wa majadiliano utafanyika Ijumaa ya tarehe (1/5/2020m) saa tatu jioni na kurushwa kwa njia ya video kwenye mitandao maalum ya chuo.

Tambua kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed ndio chuo kwa kwanza hapa Iraq kuandaa jukwaa la wanafunzi wake pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu vya kiarabu na kiajemi.

Kumbuka kuwa jukwaa hili ni sehemu ya harakati za kuimarisha mapambano dhidi ya maambukizi ya Korona, kwa kuwakutanisha wanafunzi kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: