Shamba la Firdausi linajitahidi kukidhi mahitaji ya soko la ndani la viazi mbatata na kutotegemea viazi vya kutoka nje, hususan katika mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa.
Mhandisi bwana Aadil Maliki mkuu wa shirika la Liwaaul-Aalamiyya linalo simamia mradi huo amesema kuwa: Aina ya viazi tunavyo lima inapendwa sana na walaji, vitasaidia kukidhi mahitaji ya soko la ndani na kutohitaji viazi vya kutoka nje, hususan katika mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa, ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona na kufungwa mipaka, jambo ambalo linatufanya tuwajibike kuwapatia wananchi mazao ya chakula.
Akabainisha kuwa: “Viazi hivi ni matokeo ya utafiti uliofanywa wa kupata mbegu bora yenye kutoa viazi vinavyo pendwa na walaji, tena kwa kutegemea uwezo wa ndani ambao umethibitisha mafanikio, sambamba na kutumia mbolea inayo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud ambayo haina kemikali ambazo hupunguza ubora wa mazao na kuathiri afya za walaji”.
Kumbuka kuwa shirika la Liwaaul-Aalamiyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu lilitangaza kumaliza mavuno ya awamu ya pili ya viazi mbatata, baada ya kufanikiwa awamu ya kwanza iliyo julikana kwa jina la (Uboreshaji wa viazi mbatata) ambapo ilitengenezwa mbegu bora yenye mavuno makubwa, katika juhudi za Atabatu Abbasiyya kupitia shirika tajwa, ikiwa ni miongoni mwa mkakati wa muda mrefu wa mapinduzi ya kiuchumi kwa ujumla.
Tambuwa kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inamiradi mingi ya kilimo inayo lenga kutosheleza sekta hiyo muhimu, ambayo ni mhimili wa maisha kutokana na kufungamana kwake na maisha ya binaadamu, miradi hiyo inatarajiwa kuimarisha uchumi baada ya kuanza kudhofika katika siku za hivi karibuni.