Majengo ya Shekh Kuleini yameongeza mapambano dhidi ya virusi vya Korona

Maoni katika picha
Kiongozi wa majengo ya Shekh Kuleini yaliyopo katika barabara ya (Karbala – Bagdad) bwana Ali Mahdi Swafi amesema kuwa, kazi ya kupuliza dawa kwenye maeneo mbalimbali ya majengo hayo bado inaendelea.

Akasema: “Kazi iliyo fanywa siku ya Jumamosi ilikuwa ni sehemu ya kukamilisha kazi kubwa iliyo fanywa na Ataba tukufu ya kupuliza dawa kwenye majengo yanayo tumika kutoa huduma, tumefanya kazi hiyo kwa kushirikiana na watu wa kujitolea kutoka kikosi cha Husseiniyya, tunachukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya maradhi ambukizi pamoja na virusi vya Korona, tunafanya usafi na kupuliza dawa ndani na nje ya majengo”.

Akaongeza kuwa: “Tumepuliza dawa ndani na nje ya majengo hayo, pamoja na kwenye kumbi cha chakula, za mikutano na sehemu za malazi, bila kusahau jikoni na vyooni”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imesha weta utaratibu maalum wa kupuliza dawa chini ya kamati iliyo undwa rasmi kwa ajili ya kazi hiyo, ambayo inasimamia upuliziaji wa dawa kwenye maeneo yote yanayo zunguka Ataba tukufu na majengo ya kutolea huduma pamoja na mji mkongwe na barabara za mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: