Maktaba ya wanawake imefungua jukwaa la mawasiliano kupitia Muntada-Alkafeel

Maoni katika picha
Maktaba ya wanawake ambayo ikochini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua rasmi jukwaa la mawasiliano katika Ataba tukufu chini ya anuani isemayo: (Kitengo kipya cha maktaba na utamaduni kupitia Muntada-Alkafeel ya wanawake), kwa lengo la kutoa huduma za kitamaduni na kielimu kwa wanufaika wengi zaidi, kwa namna ambayo itawawezesha kunufaika na matumizi mazuri ya mtandao, hususan katika mazingira magumu ambayo taifa linapitia kwa sasa na ulimwengu mzima.

Bibi Asmaa Al-Abaadi mkuu wa maktaba ya wanawake amesema kuwa: “Hakika hatua hii imekuja kukamilisha malengo yaliyo wekwa na maktaba katika ratiba yake ya utowaji wa huduma bora kwa wadau wake, kwa kuwa na kikao zaidi ya kimoja na kuendeleza mawasiliano pamoja nao, kwa kuwa (Muntada-Alkafeel) ni mahala muwafaka pa kujitokeza mbele ya umma, ndio tumeamua kufungua dirisha hili, (kitengo cha maktaba ya wanawake kupitia jukwaa la Muntada-Alkafeel”.

Akaongeza kuwa: “Kitengo cha maktaba ya wanawake kinatoa huduma mbalimbali za kitamaduni, wanafundisha elimu tofauti, wanatoa machapisho mbalimbali, wanaendesha mashindano ya kielimu na maarifa, dirisha hilo ni sehemu ya maktaba kujifunua mbele ya wadau wake na kuendeleza mawasiliano baina yao kwa kupitia link ifuatayo: https://forums.alkafeel.net/node/884278".
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: