Kituo cha maradhi ya ngozi katika hospitali ya Rufaa Alkafeel kimepata mtambo wa kisasa zaidi unaotibu maradhi yote ya ngozi uitwao (Yufikabina).
Daktari muhtasi wa hospitali Dokta Swaadiq Jafari amesema kuwa: “Hospitali ya rufaa Alkafeel imepata mtambo wa kisasa na vifaa muhimu vinavyo tumika kutibu aina zote za maradhi ya ngozi, mtambo huo unaitwa (Yufikabina) nao hutibu kwa kutumia mwanga, pia unatibu baadhi ya matatizo ya figo ikiwa ni pamoja na ongezeko la sumu mwilini na saratani”.
Akaongeza kuwa: “Hupangwa namna ya matibabu kutokana na hali ya mgonjwa, baadhi ya wakati mgonjwa anahitaji kutibiwa kwa mwanga pamoja na mtambo wa mwanga”.
Akafafanua kuwa: “Kituo kinatoa matibabu kwa wanaume na wanawake”.
Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inamadaktari bingwa wa maradhi tofauti, na inapokea wagonjwa wa aina zote, inamchango mkubwa sana katika sekta ya afya hapa Iraq, imesaidia kupunguza gharama za matibabu na tabu ya kusafiri nje ya taifa kwa ajili ya kutafuta matibabu.