Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinaendelea na kazi ya kupuliza dawa katika mkoa wa Karbala

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kinaendelea na kazi ya kupuliza dawa katika mkoa wa Karbala, jana jioni kimepuliza dawa katika barabara ya Mujammaáat.

Ustadh Muhammad Jamali Aáraji mjumbe wa kamati iliyo undwa na kikosi cha Abbasi amesema kuwa: “Tulianza kazi ya kupuliza dawa katika barabara ya Mujammaáat, kwa kuanzia sehemu ya mapumziko ya wanafamilia ya Hussein hadi katika duara la Dhwariba, vilevile wamemaliza kupuliza dawa pande mbili za barabara na vyombo vya usafiri vilivyo egeshwa sehemu hizo pamoja na maduka”. Akasema kuwa: “Jumla ya watu ishirini (20) waliobeba vifaa vya kisasa vyenye uwezo mkubwa wameshiriki katika kazi ya kupuliza dawa kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Korona”.

Kumbuka kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) kinaendelea kuhudumia wananchi kwa kushiriki katika program ya (Marjaiyyatu-Takaaful) au kwa kuendelea kupuliza dawa ya kujikinga na maambukizi ya Korona kwenye mikoa tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: