Shirika la uchumi Alkafeel limeanza kuvuna zaidi ya dunam (400) za ngano

Maoni katika picha
Watumishi wa shirika la uchumi Alkafeel ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wanavuna ngano na shairi katika shamba lenye ukubwa wa zaidi ya dunam (400), kwa siku moja wanavuna kiasi cha dunam (120).

Rais wa kitengo cha kilimo na mazao ya wanyama katika shirika hilo Mhandisi Ali Mazál amesema kuwa: “Kazi ya kuvuna ngano na shairi imeanza siku ya Jumapili ya tarehe (3 Mei 2020m), mazao hayo yatatunzwa katika magodauni ya wizara ya biashara katika mkoa mtukufu wa Karbala, viashiria vya awali vinaonyesha kuwa mavuno ni mazuri kama yalivyo tarajiwa”.

Akaongeza kuwa: “Ngano tunayo vuna ni miongoni mwa aina za kiiraq ambayo ni (Buhuuth/22) na (Al-Ibaa/99), nazo ni miongoni mwa aina muhimu zilizo fanyiwa majaribio miaka ya nyuma, ambapo zilionyesha kuwa na mavuno makubwa, kuhusu shairi zinazo vunywa ni za aina ya (Shairi 244) na (Shairi 9/12)”.

Akabainisha kuwa: “Zitahifadhiwa baadhi ya shairi hizo kwa ajili ya kupandwa mwakani, mabaki ya mavuno yatatumika kama chakula cha wanama wanaofugwa katika shamba la Barakaat Ardhi ya Abbasi (a.s)”.

Akasisitiza kuwa: “Lengo la kilimo hicho ni kusaidia sekta ya kilimo na kuingiza mazao katika soko la Iraq sambamba na kutumia majangwa katika kilimo na kutoa ajira kwa wananchi, pamoja na kutumia mitambo ya kisasa katika kilimo”.

Kumbuka kuwa idara ya kituo cha Saaqi na Firdausi ambazo zipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, zilikuwa zimesha tangaza kukamilika maandalizi ya kuanza kuvuna ngano, katika mashamba yenye ukubwa wa dunam (1240) huku mazao hayo yakiwa yanasubiriwa kwa ham na wizara ya kilimo kwa lengo la kuyaingiza sokoni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: