Mwezi kumi Ramadhani ni siku aliyo fariki mama wa waumini bibi Khadija (r.a)

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi kumi Ramadhani mwaka wa kumi wa utume, ndio siku aliyofariki mama wa waumini na mke wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) bibi Khadijatu Kubra (r.a), aliondoka duniani na kuacha majeraha na huzuni kubwa katika moyo wa Mtume (s.a.w.w) na umma wa waislamu kwa ujumla.

Bibi Khadija ndio mtu wa kwanza kumuamini Mtume wa Mwenyezi Mungu mtukufu, imepokewa kutoka kwa ibun Abbasi anasema: (Mtu wa kwanza kumuamini Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) katika wanaume ni Ali (a.s), na katika wanawake ni Khadija (r.a), alivumilia pamoja na Mtume (s.a.w.w) matatizo ya utume, alishirikiana na Mtume katika shughuli zake na machungu yake, alivumilia maisha ya tabu baada ya kutengwa kwake, alijitolea kila anacho miliki katika maisha yake, hakika alikuwa mfano bora kabisha kwa mwanamke muumini, bibi Khadija (r.a) baada ya kuolewa na Mtume (s.a.w.w) alikuwa na nafasi kubwa sana kwa Mtume katika kupambana na mitihani ya utume wa Mwenyezi Mungu, alimpunguzia mateso na changamoto alizokuwa anakutana nazo kutoka kwa makafiri wa kikuraishi.

Kifo cha bibi Khadija (a.s) kilikuwa bigo kubwa kwa Mtume (s.a.w.w), kwa sababu hakuwa mke tu, bali alikuwa mwanamke wa mfano kwa waumini aliye jitolea kila kitu kwa ajili ya Mtume (s.a.w.w).

Hakika alijitolea mali, heshima na utukufu, bali alijitolea nafsi yake na roho yake kwa ajili ya kumridhisha binadamu bora na mbora wa manabii na mitume, ili apate radhi za Mola wa walimwengu na utukufu wa duniani na akhera, kifo chake kilimuumiza sana Mtume (s.a.w.w) na alihuzunika sana, hadi kila mtu alitambua huzuni yake, ukizingatia kuwa kifo chake kilitokea baada ya kufariki ammi yake Abu Twalib (a.s), kutokana na ukubwa wa huzuni aliyo kuwa nayo mwaka huo ukaitwa mwaka wa huzuni, hakika tukio hilo liliumiza sana moyo wa Mtume (s.a.w.w).

Imeandikwa katika kitabu cha Anwaar Saatwia na Shajaratu Tuuba: pindi alipo fariki bi Khadija Mtume (s.a.w.w) alimuandaa na kumuosha kisha akampamba, alipotaka kumvisha sanda alikuja Jibrilu na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika Mwenyezi Mungu anakutolea salam na anakutakasia salam na utukufu, anakuambia kuwa: Ewe Muhammad hakika sanda ya bi Khadija itatoka kwetu hakika yeye alitoa mali zake zote katika njia yetu, Jibrilu akampa sanda na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hii hapa sanda ya bi Khadija amepewa na Mwenyezi Mungu kutoka peponi, Mtume (s.a.w.w) akamvisha shuka yake kwanza kisha akamvisha sanda aliyopewa na Jibrilu, akawa kavishwa sanda mbili, moja kutoka kwa Mwenyezi Mungu na nyingine kutoka kwa Mtume.

Amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa na siku aliyo kufa na siku atakayo fufuliwa. kuwa hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: