Maktaba ya wanawake inaendelea ya ratiba yake ya mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Idara ya maktaba ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutekeleza ratiba ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, iliyo andaliwa kabla ya kuingia mwezi huu, yenye vipengele vya dini na utamaduni vinavyo endana na utukufu wa mwezi huu, kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii.

Kiongozi wa idara tajwa bibi Asmaa Abadi amesema kuwa: “Katika kuenzi siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani katika mazingira ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika harakati zote hadi kwenye ratiba ya mwezi wa Ramadhani, tumeamua kutumia njia ya mitandao ya mawasiliano ya kijamii katika kuendeleza ratiba yetu”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba yetu ya mwaka huu inavipengele vifuatavyo:

  • - Usomaji wa Quráni.
  • - Mihadhara ya Dini.
  • - Nadwa za kila siku pamoja na kuzingatia matukio ya mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akaendelea kusema: “Ratiba hii inaendelea kila siku katika mwezi wa Ramadhani, tunatarajia itakuwa na matokeo chanya pamoja na mazingira magumu yaliyopo”.

Kumbuka kuwa kila mwaka katika mwezi wa Ramadhani maktaba ya wanawake huandaa ratiba maalum ambayo hutekelezwa mchana na usiku, huwa na vipengele vingi sambamba na kuadhimisha matukio ya mwezi huo mtukufu, kutokana na mazingira ya sasa pamoja na maelekezo ya Marjaa na idara za afya zilizo shauri kuepuka misongamano, sambamba na marufuku ya kutembea inayo endelea hadi sasa, ofisi ya maktaba imeamua kutumia njia hii, kwa ajili ya kuendeleza ratiba yake kwa kiwango kilekile.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: