Opresheni kubwa ya kusafisha barabara zinazo zunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha kusimamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu wanaendesha opresheni kubwa ya kusafisha barabara zinazo zunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kama sehemu ya kujiandaa na opreshini nyingine kubwa ya kusafisha barabara zote pamoja na mitaa chini ya mpango kazi uliopo.

Rais wa kitengo cha kusimamia uwanja wa katikati ya haram mbili Sayyid Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa kitengo chake kila baada ya muda fulani hufanya usafi mkubwa katika barabara na mitaa inayo elekea kwenye malalo mbili takatifu na vibaraza vyake pamoja na uwanja wake, bila kusahau usafi wanaofanya kila siku, kutokana na mazingira ya sasa ambapo mji hauna mazuwaru, tumeanza kusafisha barabara zote zinazo zunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kutumia gari na vifaa maalum vya usafi”.

Akaongeza kuwa: “Hali kadhalika tumesafisha kwenye vituo vya ukaguzi na vyooni pamoja na kuondoa misongamano, sambamba na kupamba barabara hizo kwa kupanda miti ya mauwa na kujenga kingo zake, kama sehemu ya kupendezesha mji kutokana na hadhi yake”.

Tambua kuwa siku za nyuma mkuu wa idara ya mkoa wa Karbala Mhandisi Abiir Salim Naasir na rais wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili Sayyid Naafii Ni’mah Abiis Mussawi, walitembelea barabara na mitaa kadhaa ya mji mkongwe unao zunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuangalia hali ya barabara hizo na kuweka mkakati wa kuzifafisha na kuzikarabati kulingana na mahitaji halisi ya maeneo hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: