Kwenye haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zinasomwa ziara kwa niaba na kufanya ibada maalum ndani ya mwezi huu wa Ramadhani

Maoni katika picha
Idara ya taaluma na mitandao iliyo chini kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuwa inaendelea kufanya ziara kupitia dirisha la ziara kwa niyaba kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel, kutokana na maombi ya wanaotaka kufanyiwa ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa niyaba, pamoja na kuwafanyia baadhi ya ibada za mwezi wa Ramadhani, watendaji wa ibada hizo ni masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kiongozi wa idara ya masayyid Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema kuwa: “Hakika mtandao wa Alkafeel katika kila msimu wa ibada ukiwemo mwezi mtukufu wa Ramadhani hutoa ratiba ya utekelezaji wa ibada kupitia dirisha la ziara kwa niyaba na kwenye madirisha mengine, kuhusu ratiba ya mwezi huu inavipengele vingi, miongoni mwake ni:

  • - Kufanya ziara kila siku kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Kufanya baadhi ya ibada maalum za mwezi wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kusoma Duaau-Iftitaah.
  • - Kifanya ibada za siku za Lailatul-Qadri ndani ya haram mbili takatifu.
  • - Kufanya ziara makhsusi ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwenye kumbukumbu ya kuzaliwa kwake katika mji mtukufu wa Madina.
  • - Kufanya ziara makhsusi katika haram ya kiongozi wa waumini (a.s) mbele ya malalo yake takatifu kwenye kumbukumbu ya kuuwawa kwake.

Akaongeza kuwa: “Mtu yeyote anayependa kufanyiwa ziara kwa niyaba anaweza kusajili jina lake kupitia link ifuatayo (http://alkafeel.net/zyara) katika toghuti zote za mtandao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: