Chuo kikuu cha Al-Ameed kinatumia njia ya kisasa kufundisha na kusoma kupitia mtandao (elimu masafa) wakati huu wa janga la Korona

Maoni katika picha
Rais wa chuo cha Al-Ameed Dokta Muayyad Imrani Alghazali amesema kuwa: “Katika mazingira ya (janga la Korona), imebaki namna kekee ya kusoma ni kutumia njia ya mtandao, kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya imeifanya miradi yake iendane na maendeleo ya teknolojia, inatumia njia ya kisasa zaidi ya kusoma na kujisomea kwa kupitia mtandao, imefanya hivyo baada ya kupokea maomi kutoka kwa wadau wake ya kuwataka watumie mfumo wa (elimu masafa), wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu pia ilihimiza kutumia mfumo huo ili kukamilisha selebasi ya masomo ya mwaka huu, mitandao ya mawasiliano ya kijamii inawezesha kuwafikishia wanafunzi masomo kwa urahisi na kuwafanya wakamilishe muhula wa masomo kama ilivyo pangwa”.

Akaongeza kuwa: “Tumefungua muhula wa pili wa masomo ya mwaka huu kwa kutumia njia ya mtandao, tunawahakikishia wanafunzi wetu kuwa hawatapoteza mwaka wa masomo, kumaliza masomo yao kwa wakati kutawasaidia kufikia malengo yao ya baadae, jambo hilo limetufanya tutafute namna ya kuwawezesha kutumia mtandao, tulitoa maelekezo ya kwanza ya (muongozo wa kusoma kwa mtandao katika chuo kikuu cha Al-Ameed), yaliyo muwezesha mwanafunzi kutumia mitandao ya masomo inayo tumiwa na chuo, pia tukatoa mafunzo ya utumiaji wa mitandao katika usomaji, ili kuandaa mazingira yatakayo wawezesha kusoma kwa usalama, sambamba na semina zingine za kuwajengea uwezo”.

Akabainisha kuwa: “Tunatoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na kamati ya malezi na elimu ya juu katika Ataba tukufu kwa msaada wao mkubwa, pamoja na watumishi wa chuo wakiongozwa na masayyid, wakuu wa vitengo, wakufunzi pamoja na wafanyakazi wengine wote”.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed kinatumia mfumo wa elimu masafa tangu siku za kwanza zilipo fungwa shule na taasisi za elimu hapa nchini, kutokana na sababu za kiafya ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: