Idara ya uangalizi maalum wa wagonjwa katika hospitali ya rufaa Alkafeel imesema kuwa: inavifaa vya kisasa na madaktari bingwa

Maoni katika picha
Idara ya uangalizi maalum wa wagonjwa katika hospitali ya rufaa Alkafeel imesema kuwa, inavifaa vya kisasa na madaktari bingwa pamoja na wauguzi wenye weledi mkubwa, inajopo la wataalamu wa upandikizaji pia.

Hayo yamesemwa na kiongozi wa idara hiyo Dokta Hussein Qahtwani: “Hakika idara ya uangalizi wa hali ya juu kwa wagonjwa mahutihuti ina vitanda (12), na uangalizi ya hali ya kati kuna vitanda (8), ambavyo vimewekewa mitambo ya kisasa ya kumsaidia mgonjwa kupumia pamoja na vifaa vya kusafisha figo wakati wote”.

Akaongeza kuwa: “Kitengo cha pili kinahusika na uangalizi wa hali ya kati na kuna kifaa cha uangalizi (HDU) sambamba na uangalizi maaluma wa upandikizaji wa viungo”.

Qahtwani akasema kuwa: “Hospitali ya Alkafeel imejikita katika uangalizi wa kina unao tegemea majibu ya vipimo na kiasi cha gesi”.

Akasema: “Vifaa vyote vipo na vinawawezesha madaktari kufanya upasuwaji wa aina yeyote pamoja na upandikizaji wa viungo, hadi upasuaji mkubwa kama vile wa ubongo na mwingine ambao huchukua saa (10) hadi (12) ambapo mgonjwa huhitaji vifaa vya kumsaidia kupumua na uangalizi maalum”.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hutumia madaktafi bingwa wa kimataifa katika maradhi mbalimbali, sambamba na kupokea wagonjwa wa aina zote walio katika hali zote za maradhi, hii ni hatua kubwa katika sekta ya afya hapa Iraq, imesaidia kupunguza gharama za matibabu na tabu ya kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta matibabu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: