Kwa bei nafuu: Shirika la Nurul-Kafeel linatoa kila kinacho hitajika kwenye meza ya chakula cha mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Shirika la Nurul-Kafeel linatengeneza bidhaa za chakula zenye ubora mkubwa kwa bei nafuu anayo weza kuimudu hata mtu mwenye kipato kidogo, bidhaa hizo zinapatikana kwenye vituo vya mauzo ya moja kwa moja (mubashara) vilivyopo mikowani.

Pamoja na athari zilizo sababishwa na janga la Korona katika sekta tofauti hapa nchini, shirika limehakikisha kuendelea kupatikana kwa bidhaa za chakula sokoni katika siku hizi za mwezi wa Ramadhani.

Makamo mkuu wa shirika hilo Ustadh Hamidi amesema kuwa: “Kutokana na kuingia mwezi wa Ramadhani shirika la Nurul-Kafeel limeongeza usambazaji wa bidhaa za chakula, sambamba na kudhibiti ubora katika bidhaa hizo, na kuhimiza viwanda vya juisi na maziwa kuongeza uzalishaji”.

Akaongeza kuwa: “Idara yetu imeweka mkakati wa kunufaika na uwezo wa vijana wanaofanya kazi ndani ya shirika, na kufanyia kazi fikra zao kupitia miradi inayo tumikia wananchi na kuongeza uzalishaji na pato la taifa kwa kuajiri kundi kubwa la vijana”.

Akasema: “Shirika linasambaza bidhaa zenye ubora mkubwa kupitia vituo vyake vya mauzo ya moja kwa moja vilivyopo kwenye mikoa mingi ya Iraq, na linafatilia hatua zote za utengenezaji wa bidhaa hizo, kuanzia hatua ya mwanzo kabisa hadi pindi bidhaa inapo fika mkononi kwa mlaji”.

Akasisitiza kuwa: “Tunafanya kila tuwezalo kuingiza katika masoko yetu bidhaa muhimu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, ili mwananchi apate kila anacho hitaji katika siku hizi tukufu”.

Kumbuka kuwa shirika la Nurul-Kafeel linatengeneza (linazalisha) bidhaa za chakula chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ni miongoni mwa mashirika muhimu ambayo yanategemewa na soko la Iraq kwa bidhaa za aina mbalimbali za chakula na maziwa, bidhaa zake zinaubora mkubwa na huuzwa kwa bei nafuu ambayo hata mwananchi mwenye kipato kidogo anaweza kuimudu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: