Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na makamo wake pamoja na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi wametembelea vituo kadhaa vilivyo chini yao

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na makamo wake wakiwa na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na baadhi ya marais wa vitengo, wametembelea vituo kadhaa vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamekutana na wasimamizi wa vituo hivyo na kusikiliza maelezo ya kiutendaji.

Miongoni mwa vituo walivyo tembelea ni Shirika la Khairul-Juud, shirika la Nurul-Kafeel, maegesho ya Alkafeel, na sehemu za utekelezaji wa miradi ya ujenzi ambayo ni kiwanda cha tofafi na kashi (mapambo) pamoja na nguzo.

Katibu mkuu wa Ataba tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar amesema: “Hakika ziara hii ni sehemu ya ziara endelevu zinazo fanywa na idara ya Ataba tukufu, kwa ajili ya kuangalia utendaji kazi katika vituo hivi, pamoja na kupata maelezo ya kiutendaji”.

Akaongeza kuwa: “Sehemu ya kwanza kutembelewa katika ziara hii ni shirika la Khairul-Juud, tumeangalia utendaji wake wa kazi, na kuhoji baadhi ya mambo yanayo husu uzalishaji na uuzaji, pamoja na kudhibiti ongezeko la bei katika bidhaa zinazo tengenezwa na shirika hilo”.

Akafafanua kuwa: “Kuhusu ziara yetu katika maegesho ya Alkafeel ni kwa ajili ya kuangalia utendaji wa maegesho hiyo na namna ya uingiaji na utokaji wa gari, pia tumetembelea kituo kingine kinacho jengwa ambacho kitakuwa ni kiwanda cha tofali, kashi (mapambo) na nguzo, kitakacho saidia sekta ya ujenzi nchini, kupitia bidhaa zake zitakazo kuwa na ubora mkubwa”.

Akasema: “Ziara yetu ikaishia katika shirika la Nurul-Kafeel, tumeangalia utendaji wa shirika hilo pamoja na namna ya utunzaji wa vitu, wanafuata vigezo vyote vinavyo takiwa na viwango vinavyo kubalika”.

Tambua kuwa ziara hii ni sehemu ya muendelezo wa ziara nyingi zinazo fanywa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya pamoja na makamo wake na kamati kuu ya uongozi, kwenye vituo vilivyo chini ya Ataba tukufu kwa ajili ya kuangalia utendaji wa vituo hivyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: