Yenye ubora mkuwa: Wafugaji wa nyuki Alkafeel wanaendelea kuzalisha asali kwa vifaa vya kisasa

Maoni katika picha
Wafugaji wa nyuki Alkafeel wanazalisha aina mbalimbali za asali asilia kwa kutumia vifaa vya kisasa, wanazaidi ya njia moja za uzalishaji tena njia bora na za kisasa, kupitia watumishi walio bobea katika ufugaji wa nyuki na wenye uzowefu mkubwa, pia Ataba tukufu inaipa umuhimu mkubwa sekta hii, inavifaa vyote vinavyo hitajika katika uzalishaji wa asali bora, vinavyo wezesha kutosheleza soko la ndani na kuacha kutegemea asali kutoka nje ya nchi, uzalishaji unaongezeka kila siku.

Haya ndio yaliyosemwa na kiongozi wa ufugaji wa nyuki Mhandisi Hussein Muhammad, akaongeza kuwa: “Mradi wa ufugaji wa nyuki ni miongoni mwa miradi iliyo chini ya sekta ya kilimo katika Atabatu Abbasiyya tukufu, nao unatokana na juhudi za kuimarisha uchumi wa ndani kupitia bidhaa mbalimbali, aidha ni sehemu ya kuongeza mazao ya kilimo, sambamba na kutosheleza soko la asali katika mkoa wa Karbala kwa hatua ya kwanza”.

Akabainisha kuwa: Tunazalisha asali asilia kwa asilimia %100, tena yenye aina tofauti, pamoja na kuandaa mazingira bora ya kilimo ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala, ambapo tunapanda (Kunazi, miti ya matunda, miti ya mauwa, majani ya mauwa, majani na alizeti) sambamba na miti pori ambayo husaidia nyuki katika kutengeneza asali na hupenda kutua kwenye miti hiyo.

Akafafanua kuwa: “Katika kazi hii tunatumia mbinu ya usafirishaji wa makundi ya nyuki, huwa tunazitengenezea mazingira ya kusafiri kutoka eneo moja hadi lingine kutokana na upatikanaji wa chakula chao katika mashamba yetu, hili ni jambo la pekee katika uzalishaji wa (Asali ya Alkafeel) hivyo tunavuna asali kipindi chote bila kutegemea msimu maalum”.

Akasema: Asilimia kubwa ya asali tunayo zalisha inatokana na mti wa mkunazi, ambayo inaubora mkubwa, jambo hilo linasababu nyingi, miongoni mwa sababu hizo ni kwamba Atabatu Abbasiyya imeandaa shamba maalum la mikunazi kwa ajili ya ufugaji wa nyuki.

Kumbuka kuwa kuna sehemu nne za mauzo ya asali katika mkoa wa Karbala, nazo ni:

Makao makuu.. Barabara ya Husseiniyya – karibu na kituo cha Baidhwaa.

Kituo cha mauzo mubashara chini ya kikosi cha vitalu vya Alkafeel.. barabara ya Jamhuriyyah – karibu na duka la kubadilisha pesa la Raafidiin.

Kituo namba 1.. Mtaa wa Hussein (a.s) – kwenye jengo la kibiashara Al-Afaaf.

Kituo namba 10.. katika mkoa wa Najafu Ashrafu.

Kwa maelezo zaidi piga simu namba (07718003738).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: