Mkuu wa shirika la Khairul-Juud amesema kuwa: Lengo letu ni kudhibiti mfumko wa bei na kuzalisha bidhaa zenye ubora na rafiki kwa jamii.

Maoni katika picha
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Khairul-Juud Mhandisi Maitham Bahadeli amesema kuwa: “Lengo letu ni kulinda ubora wa bidhaa zetu na ziweze kuwafikia wananchi wote kwa bei nafuu”.

Ameyasema hayo katika ziara iliyofanywa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya na makamo wake, akiwa na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na baadhi ya marais wa vitengo katika shirika hilo, akasema: “Tunawaambia wananchi wa Iraq kuwa shirika la Khairul-Juud ni shirika rafiki kwao kabla ya balaa la Korona wakati wa balaa hilo na baada yake, na hiyo ndio sera yake”.

Bahadeli akauambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Ziara iliyo fanywa na Sayyid katibu mkuu na ujumbe alio fuatana nao, ni ziara ya kukagua utendaji wa shirika, sambamba na kuangalia mazingira ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona katika hatua za uzalishaji na uuzaji, pamoja na kuangalia namna ya kutatua changamoto kama zipo, hakika kutembelea kwake katika miradi hii kunamfanya kuwa pamoja nasi katika utendaji, aidha kunatupa moyo na kututia nguvu, sambamba na kubaini haraka changamoto za kiutendaji na kuzitatua kwa wakati, jambo ambalo linaboresha utendaji, na hiyo ndio desturi ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Tambua kuwa ziara hii ni sehemu ya ziara nyingi zinazo fanywa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya pamoja na makamo wake na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi katika majengo na miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu ili kuangalia maendeleo na utendaji wa kazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: