Shirika la uchumi Alkafeel limemaliza kuvuna zaidi ya dunam (400) za ngano asilimia kubwa ya ngazo hizo zimekabidhiwa kwa wizara ya biashara

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha kilimo na ufugaji katika shirika la Alkafeel Mhandisi Ali Muzáli, ametangaza kukamilika kwa kazi ya uvunaji wa ngano na shairi katika shamba lenye ukubwa wa dunam (400) ambalo ni miongoni mwa mashamba ya shirika hilo, bado kuna zaidi ya dunam (200) hazija vunwa katika maeneo mbalimbali lakini kazi ya uvunaji kwenye maeneo hayo inaendelea.

Akaongeza kuwa: “Asilimia kubwa na ngano zilizo vunwa zimewekwa kwenye godauni za wizara ya biashara katika mji wa Karbala, tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwaka huu tumepata mavuno mazuri kama tulivyo tarajia”.

Akaendelea kusema: “Lengo la kuanzishwa mashamba haya ni kwa ajili ya kutosheleza soko la ndani kwa baadhi ya nafaka muhimu kama vile ngano na shairi, sambamba na kunufaika na ardhi ya jangwa pamoja na nguvu kazi”.

Akasema: “Ngano tuliyo vuna ni ya kiiraq, aina ya (Buhuthu/22) na (Al-Ibaa/99), mbegu hiyo ilifanyiwa majaribio katika mashamba yetu miaka ya nyuma, na ikapasishwa na vituo vya tafiti vya wizara ya kilimo, na aina ya shairi zilizo vunwa ni (shairi 244) na (shairi 12/9)”.

Akabainisha kuwa: “Kilimo cha mashamba hayo kilikuwa cha kumwagilia kwa kutumia njia bora ya umwagiliziaji”.

Kumbuka kuwa idara ya Saaqi na Firdausi zinazo husika na kilimo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu zilitangaza kukamilisha maandalizi yote ya uvunaji wa ngano katika mashamba yenye jumla ya dunam (1240), walikuwa wanasubiri wizara ya kilimo iwafungulie magodauni kwa ajili ya kuhifadhi ngano hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: