Atabatu Abbasiyya tukufu yapokea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imejaa mazingira ya furaha kufuatia maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), inayo sadifu siku ya kesho mwezi kumi na tano Ramadhani, korido na kuta zimewekwa mabango yenye jumbe nzuri, yaliyo andikwa maneno yanayo onyesha furaha kwa tukio hilo.

Makamo rais wa kitengo cha uangalizi wa haram tukufu Ustadh Zainul-Aabidina Adnani Ahmadi Quraishi, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kitengo chetu kilianza maandalizi ya maadhimisho haya mara tu baada ya kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi huu unamatukio mengi, tumeandaa mazingira muwafaka kwa kila tukio, likiwemo tukio hili la kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), watumishi wa kitengo chetu wamepamba haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wameweka mazingira ya shangwe na furaha kwa kubandika mabango na vitambaa vilivyo andaliwa na idara ya ushonaji katika Ataba tukufu, mabango na vitambaa vivyo vimeandikwa utukufu na sifa za Imamu Hassan (a.s), mapambo hayo yamewekwa kwenye mlango wa Kibla na ndani ya haram takatifu, pamoja na kufunga taa za rangi na kupamba kila kitu kilichopo ndani ya haram ikiwa ni pamoja na jukwaa la kusomea Quráni lililopo karibu na mlango wa Amiir (a.s)”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya huandaa mazingira maalum ya kusherehekea tukio hili, maadhimisho huchukua muda wa siku tatu, huwa kuna kongamano maalum la kusherehekea kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) ambalo hufanywa katika mji wa Hilla, na lingine hufanywa ndani ya haram tukufu, lakini mwaka huu kutokana na mazingira yaliyopo pamoja na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu ya kuheshimu maelekezo ya idara ya afya, ya kuepuka misongamano kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, maadhimisho ya mwaka huu yanafanywa kwa njia ya mtandao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: