Kuzaliwa kwa kipenzi cha Mtume na mjukuu wake Almujtaba (a.s)

Maoni katika picha
Katika nyumba aliyo amrisha Mwenyezi Mungu ijengwe na litajwe jina lake, imechomeza katika ulimwengu wa kiislamu nuru ya Uimamu ambao ndio muhimili wa uislamu na msingi wa Imani, nayo ni nuru ya Imamu Abu Muhammad Hassan Almujtaba (a.s) aliyezaliwa usiku wa mwezi kumi na tano Ramadhani.

Mtume (s.a.w.w) alimpokea mjukuu wake bwana wa vijana wa peponi katika mwezi wenye baraka na utukufu zaidi, hadi ukaitwa mwezi wa Mwenyezi Mungu, mwezi ambao Quráni imeteremka ndani yake, wakati wa kuzaliwa kwake ilishuhudiwa nuru ya utume na utukufu wa Uimamu.

Taarifa ya kujifungua bibi Fatuma ilipo enea, moyo wa Mtume (s.a.w.w) ulijaa furaha, akaenda haraka katika nyumba ya binti yake, kumpongeza kwa kupata mtoto pamoja na kumpongeza ndugu yake kiongozi wa waumini (a.s), alipofika (s.a.w.w), aliita: Ewe Asmaa.. niletee mtoto wangu, bibi Asmaa alimpeleka akiwa amefungwa kwenye kitambaa cha njano, Mtume akamvua kile kitambaa kisha akasema: sijakuambieni kuwa msifunge mtoto kwa kitambaa cha njano? Akasimama (w.a.w.w) akiwa mwenye furaha, akambusu na akamlisha mate yake kisha akamkumbatia kifuani kwake halafu akainua mikono na kumsomea dua ifuatayo; Ewe Mola mimi namlinda yeye na kizazi chake kutokana na shetani aliye laaniwa.

Mtume (s.a.w.w) akamfanyia taratibu za kuzaliwa kwa mtoto, akamuadhinia katika sikio la kulia na akamsomea iqama katika sikio la kushoto, maneno mazuri yalisomwa na mbora wa binaadamu katika masikio ya mtoto mtakatifu, akawa amekaribishwa duniani kwa kusomewa maneno matukufu zaidi, mwanzo gani mwema alio pata mwanaadamu zaidi ya huu aliopata mjukuu wa Mtume (s.a.w.w)?! hakika saiti ya kwanza iliyo ingia katika masikio yake ni sauti ya babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) mbora wa walimwengu, ujumbe wa sauti hiyo unasema: Allahu Akbaru, Laa ilaaha Ila-Llah.

Mtume (s.a.w.w) akamgeukia kiongozi wa waumini (a.s), akamuuliza: Je! Umempa jina huyu mtoto? Ali (a.s) akajibu: siwezi kukutangulia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Mtume (s.a.w.w) akasema: na mimi siwezi kumtangulia Mola wangu, baada ya muda mfupi akaja malaika Jibrilu akiwa na jina la mtoto kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, Jibrilu akamuambia mpe jina la Hassan.

Hakika ni miongoni mwa majina bora kabisa, kupitia jina hilo Mwenyezi Mungu alikamilisha uzuri na wema, jina hilo limechaguliwa na Mwenyezi Mungu mtukufu kama kielelezo cha uzuri na utukufu.

Hakika alikuwa na utukufu wa utume na uimamu, pamoja na utukufu wa nasaba, alifanana mno na babu yake pamoja na baba yake, hadi waumini walikuwa wanapo mtazama wanawakumbuka wazazi wake, walimpenda na kumtukuza na alikua kimbilio lao pekee baada ya matatizo yaliyo tokea katika Dini, baada ya umma wa kiislamu kuingia kwenye matatizo makubwa ambayo yalikuwa hayajawahi kushuhudiwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: