Katika usiku wa kuzaliwa ndugu yake mjukuu mkubwa: mauwa yamepambwa kwenye dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya miti na mapambo chini ya kokosi cha shamba boy wa Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamepamba mauwa kwenye dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa ndugu yake Imamu Hassan (a.s), siku aliyo zaliwa inasadifiana na siku ya kesho mwezi kumi na tano Ramadhani.

Kiongozi wa idara Mhandisi wa kilimo Ahmadi Atiyuwi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kuna wakati na siku maalumu ambazo huwa tunaweka mapambo ya mauwa yenye rangi tofauti na harufu nzuri juu ya dirisha la kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), miongoni mwa siku hizo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa ndugu yake Imamu Hassan (a.s), siku moja kalba ya maadhimisho hayo huwa tunalipamba kaburi yake takatifu kwa mauwa tuliyo lima na kuandaliwa katika vitalu vya Alkafeel, mauwa hayo huwekwa kwa umaridadi na utaalamu wa hali ya juu”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa mambo ambayo tumeyafanya katika maadhimisho haya ni kudarizi mauwa ya kijani na weupe yaliyo andikwa (Alhassan Almujtaba) yapo katika umbo la mswala, chini ya kitambaa kilicho daziziwa kuna maandishi yasemayo (Shaharu Ramadhaan), ambayo yaliandikwa tangu mwanzo wa mwezi huu mtukufu kwa aina mbalimbali za mauwa, kuna mauwa mengine ya rangi tofauti ambayo yamewekwa sehemu tofauti ndani ya haram tukufu”.

Kumbuka kuwa mauwa yote yaliyo wekwa ndani ya haram na kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), yameandaliwa na idara ya miti na mapambo yenye uzowefu mkubwa katika fani hiyo, wanaujuzi wa hali ya juu wa kupangilia mauwa na kuweka muonekano mzuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: