Idara ya hospitali kuu ya Hindiyya inatoa shukrani kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na kujenga kituo cha Alhayaat cha tatu

Maoni katika picha
Jioni ya Ijumaa mwezi (14 Ramadhani 1441h) sawa na (9 Mei 2020m) ugeni kutoka hospitali kuu ya Hindiyya ulitembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, ukakutana na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na makamo katibu mkuu pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na maraisi wa vitengo, kwa ajili ya kutoa shukrani zao kufuatia ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha tatu kilicho jengwa maalum kwa ajili ya kuwahudumia watu watakao ambukizwa virusi vya Korona katika hospitali ya Hindiyya, ujenzi uliofanywa na Atabatu Abbasiyya chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi.

Ugeni huo umeongozwa na mkuu wa hospitali Dokta Waathiqu Jayaad Fadhili Hasanawi, ambaye ametoa shukrani za dhati kwa ujenzi wa kituo hicho, kitakacho toa huduma za afya chini ya hospitali kuu ya Hindiyya.

Mjumbe wa kamati kuu ya uongozi katika Ataba Ustadh Jawaad Hasanawi amesema kuwa: “Tumekuja kutoa shukrani kwa kukamilika ujenzi wa kituo cha tatu cha Alhayaat ndani ya muda mfupi sana, siku (24) tu, kituo chenye vyumba ya wagonjwa (35)”.

Akaongeza kuwa: Ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha tatu baada ya kumaliza kituo cha Alhayaat cha pili katika mji wa Imamu Hussein (a.s) ni sehemu ya kujitolea kwa Atabatu Abbasiyya katika kusaidia kujikinga na maradhi ya kuambukiza –Allah atuepushie-.

Tambua kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu ilifanya ufunguzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya korona katika hospitali ya Hindiyya kiitwacho (kituo cha Alhayaat cha tatu) siku ya Jumapili (2 Ramadhani 1441h) sawa na tarehe (26 Aprili 2020m) mbele ya waziri wa afya wa Iraq, kisha hospitali ya rufaa Alkafeel ikakitoa kama zawadi kwa hospitali kuu ya Hindiyya.

Ujenzi wa kituo hiki ni sehemu ya kuimarisha juhudi za kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, na kupunguza msongamano katika kituo cha Alhayaat kilichopo katika mji wa Imamu Hussein (a.s), ukizingatia kuwa Hindiyya ni miongoni mwa wilaya kubwa katika mkoa wa Karbala, ipo umbali wa kilometa (20), mradi huu umefanywa kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala chini ya usimamizi wa idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: