Idara ya shule za wasichana Alkafeel inaendesha shindano liitwalo (Rauhu wa Raihanu) kwa wasichana

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati za mwezi wa Ramadhani na kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), idara ya shule za wasichana Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha shindano la (Rauhu wa Raihanu) kwa wasichana wenye umri wa miaka (6) hadi (12).

Kiongozi wa idara hiyo bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano lina sehemu tatu tofauti: sehemu ya kwanza inahusu mkarimu wa Ahlulbait (a.s) na itafungwa mwezi 22/ Ramadhani, sehemu ya pili inahusu maelezo bora, mshiriki anahaki ya kutolea maelezo picha mbili na mwisho wa kupokea maelezo hayo ni mwezi 25/ Ramadhani”.

Akaendelea kusema kuwa: “Sehemu ya tatu itakuwa ni mchoro mzuri zaidi kuhusu Imamu Hassan Almujtaba (a.s), siku ya mwisho kupokea michoro hiyo ni mwezi 27/ Ramadhani”.

Akamaliza kwa kusema: “Kutakuwa na zawadi za washindi watano wa kwanza katika kila sehemu, pamoja na zawadi nyingine kwa washiriki wote”.

Shindano hili ni sehemu ya harakati ya kitamaduni na kisanii ambayo hufanywa na idara tajwa hapo juu katika mwezi wa Ramadhani kwa ajili ya kuibua vipaji vya wasichana.

Kumbuka kuwa idara ya shule za wasichana Alkafeel ilitangaza ratiba ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuanzia siku ya kwanza ya mwezi huu.

Kushiriki katika sehemu ya kwanza ya shindano ingia kupitia link hii:

https://forms.gle/XuSX3fbsuFzLsNnR8

kushiriki katika sehemu ya pili ya shindano ingia kupitia link hii:

https://forms.gle/Vxhx76JBjDzfbUNz9

kushiriki katika sehemu ya tatu ya shindano hili tuma mchoro wako pamoja na taarifa zifuatazo: (majina yako matatu, mji, mkoa, umri, namba ya simu) kupitia but:

@musabaqa6_but.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: