Kuanzia sehemu ya Saaqi: kazi ya kuvuna dunam (1240) za ngano imeanza

Maoni katika picha
Siku ya Jumapili mwezi (16 Ramadhani 1441h) sawa na tarehe (10 Mei 2020m) watumishi wa kitengo cha Saaqi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kuvuna ngano, baada ya kukamilika maandalizi yote ya lazima, kwenye shamba lenye ukubwa wa dunam (1240), ambapo dunam (840) zipo katika mradi wa mashamba ya Saaqi huku dunam zilizo baki zikiwa katika mradi wa Firdausi ambao wataelekea kuvuna kwenye mradi huo mara tu baada ya kumaliza sehemu hii.

Mkuu wa kituo cha Saaqi Ustadh Zaki Swahibu umeuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi ya uvunaji ni sehemu ya kukamilisha kazi zilizo tangulia, shamba la Saaqi lina aina adimu za ngano za kiiraq zinazo pendwa sana, shamba hilo lina maeneo mbalimbali, eneo la Bagdadi lina dunam (360), eneo la (Ibaa/22) lina dunam (480)”.

Akabainisha kuwa: “Sehemu iliyo limwa katika eneo la Saaqi imefika dunam (840) ambazo zimegawanyika sehemu (9), sehemu (6) zinajumla ya dunam (480) zikiwa dunam (80) kwa kila kitalu, sehemu tatu zingine zimeongezwa kwenye mradi msimu huu, zinajumla ya dunam (360), zikiwa dunam (120) kwa kila kitalu, eneo hilo linamwagiliziwa kwa maji ya visima”.

Akasisitiza kuwa: “Kazi ya uvunaji huanza mapema asubuhi kila siku na huendelea hadi usiku, kisha nafaka zilizo vunwa hupelekwa katika magodauni ya wizara ya kilimo yaliyo andaliwa rasmi kwa ajili ya kuhifadhi mazao hayo, ukizingatia kuwa mradi wa Saaqi upo katika mpango wa mkoa wa Karbala”.

Kumbuka kuwa imetekelezwa ratiba kamili ya eneo lote la kilimo, kwa kufanya kilimo cha umwagiliaji chini ya shirika la teknolojia ya kilimo Khairul-Juud, na kwa kutumia mbolea inayo tengenezwa na shirika hilo yenye ubora mkubwa tofauti na aina zingine za mbolea, mbolea ambayo imeonyesha mafanikio makubwa kwa kuongeza kiwango cha mavuno.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: