Watumishi wa mabwawa ya samaki (mabwawa matano makubwa kila moja lina dunam 25) ambayo yapo chini ya shirika la uchumi Alkafeel, wanafanya usafi kwenye mabwawa hayo kwa ajili ya kuendelea na ufugaji wa samaki, kufanya hivyo ni muhimu kwa ajili ya kutengeneza mazalia ya samaki na kuwawekea mazingira bora.
Kiongozi wa idara ya mabwawa ya samaki Abdurahmaan Jaasim amesema kuwa: “Miongoni mwa majukumu ya idara inayo simamia mabwawa chini ya utaratibu wa mabwawa, tumeanza kazi ambayo hufanywa kila mwaka ya kusafisha mabwawa ya samaki na kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuweka mbegu mpya ya samaki baada ya kuvuna samaki wote kwenye mabwawa hayo”.
Akaongeza kuwa: “Jambo hili ni muhimu kwani kusafisha bwawa ni pamoja na kuondoa udongo wenye bakteria zinazo dhuru samaki na kuzuwia oksijeni jambo ambalo hufanya wapate shida katika upumuaji na kutembea ndani ya bwawa”.
Tambua kuwa mabwawa ya samaki yaliyo chini ya shirika la Alkafeel yamefanikiwa kuzalisha tani (75) za samaki mwaka jana, samaki wanao zalishwa na mabwawa hayo ni wakubwa na wenye radha nzuri, wameweza kumudu soko la walaji, hali kadhalika kituo cha kuandaa mbegu za samaki kinatoa mbegu zenye ubora mkubwa.
Kumbuka kuwa shamba la samaki linamabwawa matano makubwa, kila moja lina jumla ya dunam (25) sawa na (heka kumi na tatu takriban), yamewekewa kila aina ya zana inayo hitajika.