Watumishi wa kitengo cha kulinda nidhamu wamegawa zaidi ya vifurushi (2800) vya chakula kwa familia za wahanga wa marufuku ya kutembea katika mkoa wa Karbala

Maoni katika picha
Miongoni mwa opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) iliyo anzishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kitengo cha kulinda nidhamu katika Atabatu Abbasiyya kimegawa zaidi ya vifurushi (2800) vya chakula kwa familia za wahanga wa marufuku ya kutembea katika mkoa wa Karbala.

Wamefanya hivyo kwa ajili ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia familia za wahanga wa marufuku ya kutembea hasa wakati huu wa mwezi wa Ramadhani.

Ustadh Haidari Majhuul Muhammad ambaye ni makamo rais wa kitengo cha kulinda nidhamu amesema kuwa: “Katika kutekeleza maelekezo yaliyo tolewa na Marjaa Dini mkuu, ya kuwasaidia watu walio athiriwa na marufuku ya kutembea, watumishi wa kitengo chetu walianza kugawa chakula kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo”.

Akaongeza kuwa: “Tumegawa zaidi ya vifurushi (2800) vya chakula, ikiwemo sukari, mchele, mboga za majani na aina zingine za chakula kinacho hitajika katika mwezi wa Ramadhani”.

Akasema: “Hakika kazi za kujitolea hazisimami, bali hutakiwa kuongezeka hasa wakati wa shida”.

Kumbuka kuwa Marjaa Dini mkuu alitoa wito wa kuunganisha nguvu katika kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo wakati huu wa marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ndio Atabatu Abbasiyya tukufu ikaanzisha opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kwa ajili ya kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: