Tangazo la msiba wa Alawiyya: Ukumbi wa haram ya mtoto wake umewekwa mapambo meusi na kutangaza msimu wa huzuni za Ramadhani

Maoni katika picha
Mwezi wa Ramadhani wa mwaka wa arubaini hijiriyya kulitokea msiba mkubwa sana kwa waumini baada ya ule msiba wa kuondokewa na Mtume (s.a.w.w), nao ni msiba wa kujeruhiwa na kuuwawa kwa Imamu wa wachamungu na pambo la Dini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), tukio hilo lilipangwa na kutekelezwa na mtu muovu zaidi Abdurahmaan bun Muljim Almuradi (laana ya Allah iwe juu yake).

Kutokana na kuomboleza kumbukumbu hiyo chungu inayo anzia katika tukio la kujeruhiwa kwa kiongozi wa waumini (a.s) usiku wa mwezi kumi na nane Ramadani, kuta za malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zimewekwa mapambo meusi, kazi hiyo imefanywa na watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram takatifu, wameweka mabango yaliyo andikwa jumbe mbalimbali kuhusu tukio hilo, zimepandishwa bendera nyeusi na kuwashwa taa nyekundu kwa ajili ya kuomboleza msiba huu na kumpa pole Mtume pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: