Ibada za Lailatul-Qadr zipo aina mbili: kuna ambazo hufanywa kila siku miongoni mwa siku tatu, na kuna ambazo hufanywa katika siku maalum, Sayyid ibun Twausi ametaja katika kitabu cha Iqbaal kutoka kwa Imamu Baaqir (a.s) anasema: (Atakae huisha (fanya ibada) katika usiku wa Lailatul-Qadr atasamehewa dhambi zake hata kama zikiwa na wingi wa nyota za mbinguni au milima au bahari).
Siku hizo inatakiwa zipewe umuhimu mkubwa, atakae puuza siku hizo hatapata fadhila za usiku wa Lailatul-Qadr, kuzijali siku hizo kuna athari kubwa kwa mwanaadamu, ibada za siku hizo imegawanyika sehemu mbili:
Ibada za kila siku ya Lailatul-Qadr.
- 1- Kuoga, ni bora ukaoga wakati wa kuzama jua ili wakazi wa kuswali Magharibi na Isha uwe tayali umesha oga.
- 2- Swala ya rakaa mbili, kila rakaa baada ya kusoma Alhamdu utasoma Qul-huwa-Llahu mara saba, baada ya salam utasoma (Astaghfirullaha wa atuubu ilaihi) mara sabini.
- 3- Dua ya kufungua msahafu. Utafungua msahafu na kuuweka mbele yako halafu useme: (Allahumma innii as-aluka bikitaabika al-munzal, wa maa fiihi, wa fiihi ismukal-akbaru, wa asmaaukal-husna wa maa yukhaafu wa yurjaa, an-tajálani min utaqaaika mina nnaar) kisha umbo shida yako.
- 4- Dua ya kuweka msahafu kichwani na kumuomba Mwenyezi Mungu kwa utukufu wake. Weka msahafu kichwani na useme: (Allahumma bihaqi hadhal-Quráni, wa bihaqi man arsaltahu bihi, wa bihaqi kullu mu-uminin madahtahu fiihi, wa bihaqika alaihim falaa ahaha a’rafu bihaqika minka, bika yaa Allah –mara kumi-. Kasha sema: bi Muhammad x10, bi Ali x10, bi Fatuma x10, bil-Hassan x10, bil-Hussein x10, bi Ali bun Hussein x10, bi Muhammad bun Ali x10, bi Jafari bun Muhammad x10, bi Mussa bun Jafari x10, bi Ali bun Mussa, bi Muhammad bun Ali x10, bi Ali bun Muhammad x10, bil-Hassan bun Ali x10, bil-Hujjat x10. Kisha omba shida yako, imekuja katika hadithi kuwa utajibiwa maombi yako na kukidhiwa shida zako.
- 5- Ziara maalum ya Imamu Hussein (a.s).
- 6- Kufanya ibada katika siku tatu hizo.
- 7- Kuswali rakaa (100), hakika swala hiyo inautukufu mkubwa, na inapendekezwa katika kila rakaa usome surat Tauhidi (Qul-huwa Allahu Ahad) mara kumi baada ya Alhamdu.
Ibada maalum za usiku wa mwezi (19)
- 1- Usome: Astaghfirullaha Rabii wa atuubu ilaika, mara (100).
- 2- Usome: Allahumma il-ani qatalata Amiirilmu-Uminina, mara (100).
- 3- Usome dua isemayo: (Allahumma lakal-hamdu alaa maa wahabta lii, min intwiwaai wa maa twawaita min shahari, wa annaka lam tujin fiihi ajlii, wa lam taqtwaá umrii, wa lam tuballighunii bimaradhwin yadhurunii ilaa tarki swiyaami, walaa bisafarin yahillulii fiihil-iftwaaru, fa-anaa asuumuhu fii kifaayatika wawiqaayatika, utwiiu amraka, wa iqtaatu rizqika, wa arjuu wa uammilu tajaauzaka. Fatmim Allahumma alayya fii dhaalika ni’mataka, wajzil bihi minnataka, waslukh-hu anni bikamaali swiyaami wa tamhiswi athaami, wa ballighni aakhirahu bi khaatimati khairin wa khairahu, yaa ajwadal-mas-uuliin, wa yaa asmahal-waahibiina, wa swalla Llahu alaa Muhammadin wa aalihi twaahirina).
- 4- Kusoma dua ya: (Yaa dhaa lladhii kaana qabla kulli shaiy, thumma yabqa wa yathna kulla shaiy, yaa dha lladhii fii samawaatil-ulaa, walaa fil-aradhwiina suflaa, walaa fauqahunna walaa bainahunna walaa tahta hunna ilaahun yu’badu ghairahu, lakal-hamdu hamdan laa yaqdiru alaa ihswaaihi illaa anta, faswalli alaa Muhammad wa aali Muhammad, swalaatan laa yaqdiru alaa ihswaa-ihi illaa anta).
- 5- Kusoma dua isemayo: (Allahumma ij-al fiimaa taqdhwi wa tuqaddiru minal-Amril-mahtuum, wa fiimaa tufarriqu minal-amril-hakiim fii lailatil-Qadr, wa fil-qadhwaai lladhii laa yuraddu walaa yubaddalu, an-taktubanii min hujjaaji baitikal-haraam, almabruuri hajjuhum, almashkuuri saáyuhum, almaghfuuri dhunuubuhum, almukaffari anhum sayyiaatihim, wajál-fiimaa taqdhwi wa tuqaddiru an tutwiila umrii, wa tuwassia alayya fii rizqii, wa tafálbii kadha wa kadha).
- 6- Kusoma dua isemayo: (Allahumma innii amsaitu laka abdan daakhiran laa amliku linafsii dhwaran walaa nafán, walaa asrifu anha suuan, ash-ahu bidhaalika alaa nafsii, wa aátarifu laka bidhwafi quwwatii, wa qillati hiilatii, faswalli alaa Muhammad wa Aali Muhammad, wanjizlii maa waádtani, wa jamiia mu-uminina walmu-uminaati minal-maghfirati fii hadhihi llailah, watmim alayya maa aataitanii, fainnii abdukal-miskiinu mustakiinu, dhwaiifu, faqiiru muhiinu, Allahumma laa tajálnii naasiyan lidhikrika fiimaa aulaitanii, walaa ghaafilan li-ihsaanika fiimaa aátwaitanii, walaa aaisan min ijaabatika, wain abtwa-ata annii, fii sarraai kuntu au dhwaraai, au shiddatin au rajaai, au aafiyatin au balaai, au bu-usin au ni’maai, innaka smiiu duaa).
- 7- Dua ya mwisho katika usiku huu imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) inasema: (Subhaana man laa yamuutu, subhaana man yazuulu mulkuhu, subhaana man laa yakhfaa alaihi khaafiyyah, subhaana man laa tasqutu waraqatan illaa bi-ilmihi, walaa habbatin fii dhulumaatil-ardhi walaa ratbin walaa yaabisin illaa fii kitabi mubiin, illaa bi-ilmihi wa biqudratihi subhaanahu subhaanahu, subhaanahu subhaanahu, subhaanahu subhaanahu, maa aádhama sha-anahu, wa ajalla sultwaanahu, allahumma swalli alaa Muhammad wa Aalihi waj-alnaa min utaqaaiqa, wa suadaai khalqika bimaghfiratika, innaka anta ghafuuru rahiimu).