Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanafanya ibada za usiku wa Lailatul-Qadr kwa niyaba

Maoni katika picha
Kiongozi wa idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Haashim Shaami, amesema kuwa watumishi wa idara yake watafanya ibada za Lailatul-Qadr, kuanzia usiku wa mwezi kumi na tisa Ramadhani, kwa niyaba ya kila aliye omba kufanyiwa ibada hizo kwa kujisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net//zyara/

Akaongeza kuwa: “Kutokana na hali ya sasa ambayo hairuhusu watu kuja kwa wingi kufanya ibada za Lailatu-Qadr katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kama walivyo zowea kila mwaka, kwa sababu ya kufuata maelekezo ya marjaa Dini mkuu na muongozo wa wizara ya afya wa kujiepusha na misongamano kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akaendelea kusema: “Ibada hizo zitafanywa na watumishi wa idara yangu kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kila atakaye penda kuungana nao, watafanya katika siku muhimu ambazo ni mwezi (19 – 21 – 23) pamoja na kufanya ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Nao mtandao wa kimataifa Alkafeel kupitia dirisha la ziara kwa niyaba, umetangaza kuwa umejipanga kufanya ziara ya kiongozi wa waumini (a.s) kwa niyaba, katika siku ya kifo chake mwezi ishirini na moja Ramadhani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: