Masayyid wanafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanafanya majlisi kwa muda wa siku tatu kuanzia mwezi (19 – 21) kwa ajili ya kuomboleza kifo cha bwana wa mawasii na Imamu wa wachamungu Ali bun Abu Twalib (a.s).

Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya imefunguliwa kwa Quráni tukufu, kisha Shekh Ali Mujaan kutoka kitengo cha Dini akapanda kwenye mimbari, akasherehesha kauli ya kiongozi wa waumini (a.s) aliyo sema wakati wa kifo chake, isemayo: (Nimefuzu! Naapa kwa Mola wa Kaaba).

Kiongozi wa idara ya masayyid, Sayyid Haashim Shaami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Idara ya masayyid wanao fanya kazi katika Atabatu Abbasiyya imekuwa na kawaida ya kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) kila mwaka, kwa kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa muda wa siku tatu kuanzia mwezi (19 – 21) Ramadhani”.

Akaongeza kuwa: “Kutokana na maelekezo ya idara ya afya, mwaka huu tutakuwa na majlisi ya kuomboleza kwa ufupi, zitakazo fanyika katika ukumbi wa utawala mbele ya watumishi wachache wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akasema: “Mzungumzaji wa majlisi hizo ndani ya siku tatu atakuwa ni Mheshimiwa Shekh Ali Mujaan kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Majlisi hizi ni sehemu ya kuendelea na kuomboleza misiba iliyo wakuta watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na kuonyesha ukubwa wa misiba hiyo katika nyoyo za waumini na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Tambua kuwa idara ya masayyid hufanya maombolezo ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya tukufu kila tarehe ya kukumbuka kifo cha Imamu Maasumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: