Miongoni mwa harakati za mwezi mtukufu wa Ramadhani: Shule za wasichana Alkafeel zinafanya mashindano kwa wanawake tu.

Maoni katika picha
Idara ya shule za wasichana Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya mashindano mawili, la kwanza linaitwa (Misku najaat baina sibtu na swiraat) linahusika na Imamu Hassan (a.s), la pili ni (Mtazamo wako) linamuhusu Imamu Ali (a.s), washiriki wa mashindano hayo ni wanawake peke yao.

Kiongozi wa idara hiyo, bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Miongoni mwa harakati maalum za mwezi mtukufu wa Ramadhani, idara yetu inaendesha shindano la (Misku najaat baina sibtu na swiraat), linalo husisha maswali ya Fiqhi, Aqida na masomo mengine. Na shindano la (Mtazamo wako) linalo muhusu Imamu Ali (a.s), washiriki wa mashindano hayo ni wanawake peke yake”.

Akaongeza kuwa: “Tarehe ya mwisho ya kupokea majibu ni mwezi ishirini na tano Ramadhani, kutakuwa na zawadi ya washindi kumi wa mwanzo, pamoja na zawadi nyingine kwa washiriki wote”.

Ili kushiriki kwenye shindano maalum la Imamu Hassan (a.s) ingia katika link ifuatayo: https://forms.gle/PGhKcvnNjjg2uonK6

Na kushiriki kwenye shindano maalum la Imamu Ali (a.s).. andika mtazamo wako kuhusu picha kupitia link ifuatayo:

https://forms.gle/R2PPuU4bciacAhXu5
mashindano haya mawili ni sehemu ya harakati za idara tajwa hapo juu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa lengo la kuimarisha utamaduni wa kiislamu kwa wasichana na kuinua vipaji vyao.

Kumbuka kuwa idara ya shule za wasichana Alkafeel imesha andaa ratiba kamili ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani tangu siku ya kwanza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: