Mwezi wa Ramadhani katika kumbukumbu ya Karbala: Watu wa Karbala na uombolezaji wao wa kifo cha Imamu Ali (a.s)

Maoni katika picha
Inapoingia Alfajiri ya mwezi kumi na tisa Ramadhani, utaona nyumba za watu wa Karbala zikiwa zimewekwa mapambo meusi, huku huzuni ikionekana wazi katika nyuso za wakazi, kila mtu huelekea katika haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) kwenda kumpa pole bibi Zainab (a.s) kutokana na msiba huu mkubwa, Mwenyezi Mungu awakubalie maombolezo yao, kwa nini asiwakubalie wakati ndio usiku alio jeruhiwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), usiku ambao watu wa Karbala wamekuwa na desturi ya kuomboleza na kuweka majlisi za misiba, inapo ingia Alfajiri ya siku hiyo utasikia sauti zikisema (Wallahi nguzo ya uongofu imevunjika).

Ustadh Ali Khabaaz kiongozi wa idara ya habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu anatukumbusha namna watu wa Karbala walivyo kuwa wanaomboleza msiba huu.

Anasema kuwa: “Huzuni hutanda katika nyumba za Karbala ndani ya siku hizi, pamoja na kujishughulisha na ibada za Lailatul-Qadr lakini wamezowea kuhudhuria mihadhara ya Shekh Haadi (r.a) katika haram tukufu, kisha Shekh Mula Hamza Zaghiir, na humpa pole Imamu Hussein (a.s) kwa utaratibu walio zowea wakiwa wamejaa majonzi”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa ada walizo zowea na bado wanaendelea kufanya hadi sasa ni maukibu ya pmoja ya watu wa Karbala wa tabaka zote ambayo huelekea Najafu katika siku aliyo uwawa kiongozi wa waumini (a.s).

Siku ya mwezi ishirini; pamoja na kuendelea na majlisi za kuomboleza, watu wa Karbala hufanya jambo la kijamii, huandaa chakula maalum na kukigawa kwa mafakiri na mayatima, ni wazi kuwa kiongozi wa waumini (a.s) alikuwa baba wa mafakiri na mayatima (aliwajali sana), tunaweza kusema kuwa: jambo hili ni sehemu ya kufuata mwenendo wa Imamu Ali (a.s), watu wengi wa Karbala hupika chakula mwezi ishirini Ramadhani na kukigawa kwa mafakiri na mayatima”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: